Bado tuko wote kwenye Programu yetu ya TANZANIA TUWEKEZE. HAIPPA PLC tupo kujenga Uchumi usioyumba sio tu mtu kwa mtu mmoja mmoja bali kwa familia na Taifa kwa ujumla. Mara nyingi utasikia serikali mbalimbali duniani zikiweka mikakati na jitihada za kuvutia Wawekezaji. Hii inakupa picha jinsi Uwekezaji ulivyo jambo la muhimu duniani. Nakukumbusha kwamba PROGRAMU hii ya kibingwa ya TANZANIA TUWEKEZE inaletwa kwako na HAIPPA PLC.
Kwa wanafunzi wetu wapya, HAIPPA PLC ni Kampuni ya Umma inayofanya shughuli za kubuni Miradi ya Uwekezaji jumuishi sambamba na Kuelimisha na Kushauri Umma kuhusu mambo ya Hisa na Uwekezaji. Leo tujadili pamoja kwanini HISA ni UFUNGUO MAMA WA NDOTO ZAKO KIUCHUMI.
Tuanze kwa Kujikumbusha HAIPPA Tunaposema Hisa Tunamaanisha nini?
Kwa lugha rahisi kabisa HISA ni dhamana ya kifedha (financial instrument) inayokupa haki ya kuwa na umiliki kwenye kampuni. Unaponunua Hisa unanunua sehemu ya Kampuni na unakuwa mmoja wa watu wanaomiliki hiyo Kampuni na biashara zake.
Tutazame sasa kwanini HAIPPA tunaamini Hisa ni Ufunguo Mama katika Uchumi wa Mtu mmoja mmoja, Familia naTaifa. Tuanze na Faida kwa Mwekezaji mmoja mmoja:
Faida zote hizi zinabainisha msimamo wa HAIPPA PLC kwamba Hisa ni Ufunguo wa Mama katika Uchumi wa Mtu, Familia na Taifa. Sasa tupigie mstari baadhi ya Mambo ambayo ni muhimu kufahamika kwa Mwekezaji anayeanza kujifunza kuhusu Uwekezaji.
Ni Kampuni Gani zinaruhusiwa Kuuza Hisa zake kwa Umma?
Kampuni zinazoruhusiwa kuuza hisa zake kwa Umma ni zile ambazo katika Usajili wake zimepewa hadhi ya kuwa Kampuni za Umma yaani Public Limited Company au kwa kifupi PLC.
Tunapata wapi Taarifa kuhusu Kampuni za Kuwekeza?
Taarifa kuhusu Kampuni za kuwekeza hupatikana kupitia Masoko ya Hisa na Kampuni changa au mpya taarifa zake hupatikana kupitia website za Kampuni husika, vyombo mbalimbali vya Habari au madalali wa Hisa.
Masoko ya Hisa ni Kitu Gani?
Masoko ya Hisa ni majukwaa ambapo Hisa za Makampuni mbalimbali huuzwa na kununuliwa.
Je Kampuni zote za Hisa zipo kwenye Masoko ya Hisa?
Hapana sio Kampuni zote za Hisa zipo kwenye Masoko ya Hisa. Kampuni changa au mpya nyingi hazipo kwenye Masoko ya Hisa.
Sheria zinasema nini Kuhusu Kampuni za Umma kuwepo kwenye Masoko ya Hisa?
Sheria hailazimishi Kampuni ya Umma kuwepo kwenye Soko la Hisa kwasababu Kuorodhesha hisa za Kampuni kwenye Soko la Hisa sio lazima ni hiari kabisa na Lini zitaorodheshwa yanabaki kuwa Maamuzi ya Bodi na Wanahisa wa Kampuni husika.
Je ni Salama kuwekeza kwenye Kampuni za Umma ambazo hazipo kwenye Masoko ya Hisa?
Jibu ni ndiyo. Ni salama kuwekeza kwenye Kampuni ya Umma hata kama Hisa zake hazipo kwenye Soko la Hisa. Mambo ya kuzingatia ni Kampuni husika iwe imesajiliwa kama ni Kampuni ya Umma na maono na biashara za Kampuni husika zinalandana na malengo yako kwamba ni ya muda mfupi au muda mrefu. Kwenye kuchagua Kampuni ya Kuwekeza Wawekezaji hugawanyika katika makundi mawili; Wawekezaji wanaopenda Hisa za Makampuni makongwe yaliyo na muda mrefu sokoni hata kama zinalipa faida ndogo. Kundi la pili ni Wawekezaji wanaopenda Kampuni zinazokua haraka na kulipa faida nzuri hata kama ni changa au mpya sokoni. Kundi hili la pili hupendelea kununua hisa za Kampuni kabla au wakati wa kutambulishwa kwenye masoko ya Hisa.
Kwanini Watanzania wengi Hawajachangamkia Uwekezaji kwa njia ya Hisa?
Kwa utafiti uliofanywa na HAIPPA PLC unaonyesha ziko sababu kadhaa zilizosababisha Watanzania wengi kushindwa kuwa kwenye Uwanja wa Uwekezaji kwa njia ya hisa.
a) Watanzania wengi hawajafundishwa na hawaelewi kabisa kitu Hisa wala Uwekezaji na wengi wamekuwa katika imani kwamba 'Mwekezaji ni Mtu tajiri'. Ukweli ni kwamba hata ukiwa na Tsh20,000 unaweza kuanza safari yako ya kuwa Mwekezaji.
b) Tanzania bado tuna uchache wa Makampuni ya Hisa.
c) Wawekezaji wadogo waliowahi kuthubutu kuwekeza kabla kukaa muda mrefu bila kupata Gawio wala taarifa kutoka kwa Kampuni zao kuhusu maendeleo ya Uwekezaji wao.
d) Wengi kwa kutokujua jinsi ya kupima faida za Uwekezaji hutumia gawio kama kipimo cha kuchagua kampuni na huacha faida na vipimo vingine kama vile ongezeko la mtaji kupitia bei ya Hisa.
HAIPPA PLC Tunafanya nini Kuchangamsha Uwekezaji nchini?
HAIPPA PLC tumeanzisha Akademi ya Uwekezaji na Programu ya Tanzania Tuwekeze ili kutoa mafunzo ya Uwekezaji kwa Vitendo. Kupitia Program hii kila Mtanzania anapata fursa ya kufungua Akaunti ya HAIPPA bila gharama na kununua Hisa za awali kati ya 50 na 1000. Ili kuongeza mvuto tumefanya ubunifu, Gawio la HAIPPA linalipwa kila mwezi kiwango cha 3% na linalipwa kwa njia ya Hisa mpya ambazo unaweza kuziuza na kujipatia fedha taslimu . Kuhusu taarifa kwa Wawekezaji HAIPPA PLC tunatoa taarifa za kutosha kupitia mifumo ya kidigitali na vituo vyetu vya Huduma kwa wateja. Ili kukabiliana na Tatizo la uchache wa Makampuni ya Uwekezaji, HAIPPA tunasaidia kubuni Makampuni mapya na Miradi mipya ya Uwekezaji jumuishi kwenye Sekta mbalimbali ili kupanua wigo kwenye Uwanja wa Uwekezaji.
Nini Wito wa HAIPPA PLC kwa Umma?
HAIPPA PLC tunawaalika Watanzania kufungua akaunti za HAIPPA ili kujipatia elimu, taarifa na fursa mbalimbali zinazojili kwenye dunia ya Uwekezaji. Kauli mbiu yetu HAIPPA tnasema Kila Mtanzania Sasa ni Mwekezaji.
Mawasiliano
Tunakukumbusha Umma kwamba Akaunti ya HAIPPA na Elimu ya awali vinatolewa bure. Huduma zetu zinapatikana Mikoa yote kupitia simu yako iwe kubwa au ndogo. Kupata Elimu zaidi, Kufungua Akaunti na Huduma zetu
Tutembelee www.Haippa.net
Jaza fomu ya Kujiunga https://in.haippa.co.tz/authentication/signup
Au Piga *149*46*23# au Simu 0755947943; App yetu Play store ni HAIPPA PLC
Ofisi zetu zipo DSM (Kisutu), Mwanza (Nyamanoro) na Mara (Mwembeni Complex Musoma Mjini). Pia tuna Mawakala Mikoani
KARIBUNI HAIPPA
Akademi ya Uwekezani Tanzania, Fursa za Uwekezaji kwa Wote
WEKEZA KWA KUJIAMINI
HUDUMIWA KIDIGITALI UKIWA POPOTE!