Taarifa rasmi ya Shirika la Finscope ya mwaka 2023 inabainisha wazi kwamba Watanzania watu wazima wanaoshiriki fursa za Masoko ya Hisa ni 0.51%. Taarifa hii kwa lugha rahisi inabainisha kwamba kila watanzania 200 watu wazima kuna mtu mmoja tu ndiye anayeshiriki fursa za Uwekezaji kupitia masoko Hisa. Hali ikoje kwenye nchi zingine? Marekani wako na 60%, Singapore 48%, Korea Kusini 40%, China na India ni 24%. HAIPPA PLC kupitia Akademi yetu ya Uwekezaji tunatekeleza Programu ya TANZANIA TUWEKEZE. Mradi huu unalenga kuwaleta Watanzania Milioni 20 kwenye fursa za Uwekezaji kwa njia ya Hisa sambamba na Kuwajenga Watanzania Milioni moja kuwa Matajiri wa Hisa na Wawekezaji wakubwa. Makala ya leo tunabainisha kwanini Hisa ina Upekee katika Uwanja wa Uwekezaji.
HAIPPA PLC Tunaposema Hisa Tunamaanisha nini?
Kwa lugha rahisi kabisa Hisa ni dhamana inayokupa umiliki kwenye kampuni. Unaponunua Hisa unakuwa mmoja wa Watu wanaomiliki Kampuni husika na unapata haki ya kuwa Mnufaika wa faida, mali na thamani inayotokana na Ukuaji wa hiyo Kampuni.
HAIPPA PLC Tunaposema Kampuni ya Hisa Tunamaanisha Nini?
Kampuni ya Hisa ni Kampuni au biashara inayomilikiwa na watu wengi. Kwa lugha nyingine Kampuni za Hisa huitwa Kampuni za Umma na kwa mujibu wa Sheria za Tanzania Kampuni ikiwa na Wamiliki wanaozidi 50 basi automatiki hiyo inatambuliwa kuwa ni Kampuni ya Umma na inapaswa kutambulishwa ikiwa na neno PLC mbele yake ikimaanisha Public Limited Company kama ilivyo HAIPPA PLC. Kuna aina mbili za Kampuni za Hisa yaani PLC. Kampuni ambazo hisa zake zinauzwa kupitia Masoko ya Hisa yaani Listed PLC na Kampuni ambazo Hisa zake hazijaorodheshwa kwenye Masoko ya Hisa yaani Unlisted PLC.
Masoko ya Hisa ni Kitu Gani?
Masoko ya Hisa ni majukwaa ambapo Hisa huuzwa na kununuliwa hapa Tanzania mfano wake ni Soko la Hisa la Dar es Salaam kwa kifupi DSE. Hapa ni mahali ambapo mtu unaweza pia kupata Taarifa mbalimbali za Makampuni ambayo ni Listed PLC. Taarifa kuhusu Unlisted PLC utazipata kupitia jitihada zako binafsi.
Kwanini baadhi ya PLC Hisa zake Hazipo kwenye Masoko ya Hisa?
Sababu za msingi ziko kama tatu kwanini baadhi ya Kampuni Hisa zake Hazipo kwenye Masoko ya Hisa:
1. Ni Maamuzi ya Bodi ya Kampuni kwamba hisa zao hazitaorodheshwa kwenye Masoko ya Hisa. Ni muhimu kufahamu kwamba Kuorodhesha hisa kwenye Soko la Hisa sio lazima ni hiari kabisa na Lini zitaorodheshwa yanabaki kuwa Maamuzi ya Bodi na Wanahisa wake.
2. Kampuni Changa. Zoezi la kuzifanya hisa za Kampuni ziwepo kwenye Soko la Hisa huhusisha gharama kubwa hii husababisha Kampuni changa kuchelewa kupeleka Hisa zake kwenye Soko la Hisa.
3. Masharti ya Soko la Hisa ambayo ni pamoja na Kiwango cha Wanahisa Waliokwisha jiunga na Kampuni, Kiwango cha Mtaji uliojengwa kabla ya kuorodheshwa na kipindi ambacho Kampuni hiyo imefanya biashara kabla ya kupeleka hisa zake sokoni. Mfano Soko la Hisa la DSE moja ya Masharti ni Kampuni iwe angalau na Wanahisa 1000 kabla ya Kuorodheshwa Sokoni, iwe na Mtaji usiopungu shillingi Bilioni moja na iwe imefanya biashara angalau miaka mitatu.
Kuna Kitu kinaitwa Magari ya Uwekezaji hiki ni Kitu gani?
Kwenye Uwanja wa Uwekezaji kuna aina mbalimbali za Magari ya Uwekezaji. Magari ya Uwekezaji tunamaanisha mahali ambapo unaweza kuweka mtaji wako kwa lengo la kuulinda, kuukuza na kupata faida. Pote duniani Magari maarufu ya Uwekezaji ni pamoja na Hatifungani (Bonds), Hisa, Mifuko ya Pamoja kama UTT, Ardhi/Majengo na Biashara Binafsi. Huko mbele tutapata fursa ya kujifunza kuhusu gari moja moja lakini kwa leo tutajikita zaidi kwenye Uwekezaji kwa njia ya Hisa.
Hisa zina Miujiza au Upekee Gani Tofauti na Magari mengine?
Kama tunavyosema Hisa zina Miujiza au Upekee mkubwa sana unapofanya malinganisho na Magari mengine ya Uwekezaji.
HAIPPA tumejaribu Kutambua Maeneo 12 ambayo yanafanya Uwekezaji kwa njia ya Hisa kuwa na Upekee:
Kwanini Watanzania wengi hawafuatilii Fursa za Uwekezaji kwa njia ya Hisa?
Kwa utafiti uliofanywa na HAIPPA PLC ziko sababu kadhaa zilizosababisha Watanzania wengi kushindwa kuwa na umiliki wa hisa kwenye Makampuni
a) Watanzania wengi hawajafundishwa hii elimu na hawaelewi kabisa kitu Hisa wala Uwekezaji na wengi wamekuwa katka imani kwamba 'Mwekezaji ni Mtu tajiri'. Kumbe hawajui hata ukiwa na Tsh5,000 inatosha kwa Mtu kuanza kuwekeza.
b) Uchache wa Makampuni ya Hisa nchini. Soko la Hisa la Tanzania lina makampuni 28 tu yaliyoorodheshwa, wakati Marekani ina makampuni ya Hisa 6000+, China ina Makampuni 4500+ na India ina Makampuni 5500+
c) Wawekezaji kukaa muda mrefu bila kupata taarifa kutoka kwa Kampuni zao kuhusu maendeleo ya Uwekezaji wao. Baadhi ya Makampuni kushindwa kutoa Gawio kwa muda mrefu kwa Wanahisa wake na mengine kutoa faida ndogo sana. Hali hii hupoteza mvuto kuwafanyawatu wengi kuona kama Hisa sio biashara.
d) Wengi kwa kutojua hupima faida ya Uwekezaji kwa kutumia gawio badala ya Faida kubwa inayotokana na ongezeko la Mtaji Hisa inapopanda bei.
HAIPPA PLC Tunafanya nini Kupunguza ukubwa wa Tatizo?
HAIPPA PLC tumeanzisha Akademi ya Uwekezaji. Hiki ni Chuo maalum cha mafunzo ya Uwekezaji kwa Vitendo. Watanzania wanapata fursa ya kufungua Akaunti ya HAIPPA bila gharama na kununua Hisa kati ya 50 na 1000 ambazo wanaweza kuziuza wakati wowote baada ya miezi mitatu. Ili kuongeza mvuto tumefanya ubunifu, Gawio la HAIPPA linalipwa kila mwezi kiwango cha 3% na kinalipwa kwa njia ya Hisa mpya. Kwa kuwa HAIPPA PLC bado haijaorodhesha hisa zake kwenye Soko la Hisa, Bei za hisa za HAIPPA hupangwa na Kampuni hivyo kupunguza hatari ya hisa kushuka bei na hii huwahakikishia wawekezaji kwamba watapat faida. Ili kukabiliana na Tatizo la uchache wa Makampuni, HAIPPA tuna Malengo ya kusaidia kuanzisha Makampuni mapya ya Umma kwenye Sekta mbalimbali ili kupanua wigo kwenye Uwanja wa Uwekezaji.
Tujikumbushe kwa Kifupi HAIPPA PLC ni Nani?
HAIPPA PLC ni Kampuni ya Umma (Kampuni ya Kijamii) inayofanya shughuli za Kubuni Majukwaa na Miradi ya Uwekezaji jumuishi yaani uwezekaji unaowapa fursa wananchi wengi kushiriki.
HAIPPA PLC Wanafanya Shughuli Gani hasa?
HAIPPA PLC Shughuli zetu kuu ni Kubuni na Kujenga Majukwaa na Miradi kwa ajili ya Umma kuwekeza.
HAIPPA PLC Tunaona Tatizo Gani kwenye Sekta ya Uwekezaji
Nchini Tanzania na sehemu kubwa ya bara letu la Afrika takribani asilimia 99 ya Watu Wazima Hawashiriki kwenye Fursa zinazotolewa Kupitia Masoko ya Hisa na Uwekezaji wa Umma. Hali hii inatupunguzia ustawi wa kiuchumi na kijamii kama mtu mmoja mmoja, familia na Taifa.
HAIPPA PLC Tumekuja na Suluhisho Gani?
HAIPPA PLC kama Kampuni ya Umma (Kampuni ya Kijamii) tunabuni, tunanzisha na tunajenga Majukwaa na Miradi ya Uwekezaji jumuishi na kuwapa fursa umma (wananchi) kununua hisa na kuwekeza kwenye miradi hiyo. (Inclusive Public investment platforms)
Nini hasa Dhamira ya HAIPPA PLC?
Dhamira yetu ni kuendeleza Ustawi wa Watanzania Kupitia uwekezaji wa pamoja unaowajumuisha wote, kwa kutoa majukwaa salama, rahisi, na yenye uwazi yanayowawezesha kila mtu kuwekeza, kujenga Uchumi wake, na kuchangia maendeleo ya jamii na Taifa.
Nini Wito wa HAIPPA PLC kwa Umma?
Wito wetu kwa Umma tunawaalika kufuatilia kwa karibu shughuli na Fursa za HAIPPA PLC na kufungua akaunti za HAIPPA ili wasipitwe na elimu, taarifa na fursa mbalimbali zinazojili kwenye dunia ya Uwekezaji. kauli mbiu yetu inasema Kila Mtanzania Sasa ni Mwekezaji.
Mawasiliano
Elimu Zaidi, Kufungua Akaunti na Kuwekeza Tutembelee www.Haippa.net
Au Piga *149*46*23# au Simu 0755947943; App yetu Play store ni HAIPPA PLC
Ofisi za HAIPPA zipo DSM (Kisutu), Mwanza (Nyamanoro) na Mara (Mwembeni Complex Musoma Mjini)
Pia Huduma zetu zinapatikana kupitia kwa Mawakala wetu Mikoa mbalimbali
KARIBUNI HAIPPA
Akademi ya Uwekezani Tanzania, Fursa za Uwekezaji kwa Wote
WEKEZA KWA KUJIAMINI